• SURA YA PILI : MADA KUU 2: LUGHA NA MATUKIO YA KIJAMII NA KITAIFA

    MADA NDOGO: Sikukuu, sherehe na matukio ya kitaifa nchini Rwanda 
    SOMO LA 7: Sikukuu, sherehe na matukio ya kitaifa katika kalenda

    7.1 Kifungu kuhusu sikukuu sherehe na matukio ya kitaifa nchini Rwanda

    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni kalenda hii ya mwaka wa
    2016 kisha mjadiliane kuhusu tarehe maalum za sikukuu na matukio rasmi ya

    Kitaifa:


    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni picha hizi kisha msome
    kifungu cha habari kinachofuata kuhusu sikukuu, sherehe na matukio ya
    kitaifa nchini Rwanda. Baada ya kusoma kifungu, mjibu maswali ya ufahamu

    yanayofuata.



    Maswali ya ufahamu

    1. Taja sherehe ambayo husherehekewa mwanzoni mwa mwaka.
    2. Taja sherehe ambayo husherehekewa mwishoni mwa mwaka.
    3. Ni tukio gani ambalo huadhimishwa tarehe saba mwezi wa Aprili
    nchini Rwanda?
    4. Ni sherehe gani ambayo hukumbukwa tarehe moja mwezi wa Februari
    nchini Rwanda?
    5. Ni sherehe gani ambayo huadhimishwa tarehe moja mwezi wa Julai
    nchini Rwanda?
    6. Taja sherehe mbili ambazo huadhimishwa na Wakristo.
    7. Taja sherehe mbili ambazo huadhimishwa na Waislamu.
    8. Sherehe ya Umuganura huadhimishwa mwezi gani?

    9. Sherehe ya Krismasi ni sikukuu ya dini gani?

    7.2 Msamiati kuhusu sikukuu nchini Rwanda

    Kutokana na kifungu cha habari mlichosoma hapo awali, katika makundi ya
    wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu maana ya msamiati mpya uliojitokeza
    unaohusiana na sherehe na sikukuu nchini Rwanda. Kamusi ya Kiswahili inaweza

    kutumika inapohitajika.

    Kwa mfano:

    serikali: mfumo au chombo chenye mamlaka ya kutawala nchi au eneo

     fulani.

    Zoezi la 7.1

    A. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni maana
    ya msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi hizi. Tumieni kamusi
    panapohitajika.
    1.Wanyarwanda walipigana dhidi ya wakoloni.
    2.Wananchi hawafai kutumia mabavu wanapotafuta mali.
    3.Nchi yetu ilipata ukombozi miaka mingi iliyopita.
    4.Serikali yetu ina viongozi wazuri.
    5.Utawala wa rais wetu ni wa kuigwa na viongozi wengi duniani.
    B. Katika makundi yenu, tungeni sentensi sahihi kwa kutumia maneno

    yaliyopigiwa mistari katika sentensi za zoezi la 1A.

    Zoezi la 7.2

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jazeni nafasi zilizo wazi katika

    sentensi hizi kwa jibu sahihi kutoka katika mabano. 

    1. Sherehe za mwaka mpya ________________ mwanzoni mwa kila
    mwaka. (huathimishwa, huadhimishwa)
    2. Rwanda ni ____________________ inayopendwa na watu wengi
    ulimwenguni. (inchi, nchi)
    3. ____________ ya Krismasi hufanyika tarehe 25 mwezi wa Disemba.
    (Shehere, Sherehe)
    4. Siku ya ______________ husherehekewa tarehe 1 mwezi wa Februari.
    (washujaa, mashujaa)
    5. ______________ husherehekewa wiki ya kwanza mwezi wa Agosti.

    (Umagunura, Umuganura)

    7.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mjadili kuhusu
    sherehe na sikukuu nchini Rwanda. Waeleze wenzako:
    1. Shughuli zote zinazofanyika katika sherehe za mwaka mpya.
    2. Nguo unazopenda kuvaa unapoenda katika sherehe za harusi.
    3. Sikukuu unayopenda kuadhimisha katika kalenda. Toa sababu.
    4. Umuhimu wa sikukuu na sherehe mbalimbali kwa Wanyarwanda.

    5. Umuhimu wa kuwa na Kalenda rasmi nyumbani.

    7.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni na muigize mchezo mfupi
    kuhusu sikukuu nchini Rwanda. Mwanafunzi mmoja amuulize mwenzake maswali

    mbele ya darasa, naye ajibu vizuri.

    Mfano wa mazungumzo:

    Kamana: Habari dada Mukamana.
    Mukamana: Salama kaka.
    Kamana: Sikukuu ya Uhuru huadhimishwa lini?
    Mukamana: Sikukuu ya Uhuru huadhimishwa tarehe mosi mwezi wa Julai
     kila mwaka.

    Kamana: Ooh! Nimekumbuka. Asante sana dada

    Zoezi la imla

    Funga kitabu chako kisha ufungue daftari lako na uandike kwa usahihi

    maneno au vifungu vya maneno ambayo mwalimu wako atakusomea.

    7.5 Sarufi: Matumizi ya wakati uliopita 

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro hii ya masimulizi
    mafupi yafuatayo kisha kila mmoja awasimulie wenzake alivyosherehekea mwaka

    mpya uliopita. 

      

    Katika sherehe za mwaka mpya uliopita, niliamka mapema, nikaoga,
    nikapiga mswaki, nikavaa nguo mpya na kunywa kiamshakinywa. Baadaye
    niliondoka na kuelekea kijijini kumtembelea kaka yangu. Nilipofika huko
    kijijini, niliwaona watoto wengi wakicheza kandanda katika uwanja mdogo.
    Nilijiunga nao. Baada ya dakika chache, mwamuzi wa mchezo huo alipuliza
    kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo huo. Timu ya Mashujaa ilipata

    ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya timu ya Simba.

    Swali: Eleza wakati uliotumika katika masimulizi mliyosoma hapo juu pamoja

    na masimulizi yenu kwa kutoa mifano ya vitenzi vilivyotumika.

    Zoezi la 7.3

    A. Orodhesha vitenzi vyote vilivyotumika katika masimulizi mliyoyasoma
    hapo awali.

    B. Tambua nyakati zilizotumika katika vitenzi mlivyoorodhesha

    Maelezo muhimu!

    Funga kitabu chako kisha ufungue daftari lako na uandike kwa usahihi

    maneno au vifungu vya maneno ambayo mwalimu wako atakusomea.

    7.5 Sarufi: Matumizi ya wakati uliopita

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro hii ya masimulizi
    mafupi yafuatayo kisha kila mmoja awasimulie wenzake alivyosherehekea mwaka

    mpya uliopita. 


    Swali: Eleza wakati uliotumika katika masimulizi mliyosoma hapo juu pamoja

    na masimulizi yenu kwa kutoa mifano ya vitenzi vilivyotumika.

    Zoezi la 7.3

    A. Orodhesha vitenzi vyote vilivyotumika katika masimulizi mliyoyasoma
    hapo awali.

    B. Tambua nyakati zilizotumika katika vitenzi mlivyoorodhesha.

    Maelezo muhimu!

    Wakati uliopita huonyesha matukio ambayo huwa tayari yameshatendeka.
    Wakati uliopita hutumia kiambishi cha wakati -li-. Kiambishi hiki hutumika
    katika nafsi zote za Kiswahili.
    Kiambishi -ka- hutumika katika sentensi iliyo na matukio yanayofuatana

    katika wakati uliopita.

    Mifano:
    1. Nilitembea pamoja na kakangu.
    2. Aliamka akavaa nguo za michezo.
    3. Mimi nilipika chakula, nikala na kulala.
    4. Dereva aliwasha gari, akaliendesha haraka na kushikwa na polisi.
    5. Sisi tulivuna mahindi wiki iliyopita.
    Katika masimulizi ya wakati uliopita, maneno kama vile: halafu, kisha na

    baadaye hutumika.

    Zoezi la 7.4

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jazeni nafasi zilizo wazi katika

    sentensi zinazofuata kwa kutumia wakati uliopita. 

    Kwa mfano: Mama __________ (fua) nguo, __________ (pika) na
     ________ (fagia) nyumba.
    Jibu: Mama alifua nguo, akapika na kufagia nyumba.
    1. Kaka __________ (oga), __________ (piga) nguo pasi na _________
    (enda) shuleni.
    2. Mtoto __________ (kunywa) maziwa, __________ (bembelezwa) na
    __________ (lala).
    3. Mwanafunzi ____________ (enda) shuleni, ____________ (soma) na
    __________ (fanya) mtihani.
    4. Ng’ombe ____________ (kula) nyasi, ____________ (kunywa) maji
    na __________ (rudi) zizini.
    5. Mmea _____________ (pandwa), ____________ (wekewa) mbolea

    na __________ (nyunyiziwa) maji.

    Zoezi la 7.5

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, badilisheni sentensi hizi ziwe
    katika wakati uliopita.

    1. Mama anapika wali.

    2. Mimi nitaenda shule.
    3. Kwa nini unalia?
    4. Siku ya sherehe ya Krismasi imefika.

    5. Wanyarwanda wanaadhimisha siku ya Mashujaa.

    Zoezi la 7.6

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha mtunge sentensi

    tano sahihi kwa kutumia wakati uliopita ukitanguliza msamiati ufuatao

    Kwa mfano: Tarehe

    Tarehe moja mwezi wa Februari tuliadhimisha sikukuu ya Mashujaa.
    1. Uhuru
    2. Ukombozi
    3. Ukoloni
    4. Utawala

    5. Siasa

    7.6 Sarufi: Matumizi ya wakati ujao

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tazameni mchoro wa kifungu
    kifuatacho kisha kila mmoja asimulie anavyopanga kusherehekea mwaka mpya

    ujao baada ya kusoma kifungu mlichopewa kwenye ukurasa unaofuata. 



    Swali: Eleza wakati uliotumika katika masimulizi mliyosoma hapo juu pamoja

    na masimulizi yenu kwa kutoa mifano ya vitenzi vilivyotumika.

    Zoezi la 7.7

    A. Orodhesha vitenzi vyote vilivyotumika katika masimulizi mliyoyasoma
    hapo awali.

    B. Tambua nyakati zilizotumika katika vitenzi mlivyoorodhesha.

    Zoezi la 7.8

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizo wazi kwa

    vitenzi vilivyo kwenye mabano katika wakati ujao.

    Katika sherehe za Pasaka za mwaka ujao, Kamana ____________ (enda)

    kanisani kwa ajili ya ibada. Baadaye, __________ (tembelea) marafiki

    zake na kusherehekea pamoja nao. Kisha jioni ________________ (rudi)

    nyumbani. Ndugu yake Yusufu ______________ (pokea) kwenye kituo

    cha basi. Halafu ____________ (enda) nyumbani pamoja.

    Zoezi la 7.9

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni aya moja sahihi yenye

    kuhusisha matukio ya wakati ujao.

    Zoezi la 7.10

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, badilisheni sentensi zinazofuata

    ziwe katika wakati ujao.

    Kwa mfano: Mwalimu anaandika ubaoni.
    Jibu: Mwalimu ataandika ubaoni.
    1. Mwanafunzi huyu anasoma kitabu cha hadithi.
    2. Mbuga hii ilifunguliwa na rais wetu.
    3. Darasa letu limesafishwa na wanafunzi hawa.
    4. Kwa nini mnanunua vitabu vingine?

    5. Wanyamapori hawa wanakula nyasi.

    Maelezo muhimu!

    Wakati ujao hutumiwa kuonyesha matukio ambayo huwa yanatarajiwa
    kutendeka. Wakati huu hutumia kiambishi -ta-. Kiambishi hiki hutumika

    katika nafsi zote za Kiswahili.

    Mifano:
    1. Nitaomba walinzi wa mbuga waniongoze na baadaye nitapiga picha.
    2. Nitavaa kanzu nzuri halafu nitaenda msikitini kusali.
    3. Mwalimu atatufundisha kesho kisha atatupa mtihani.
    4. Sherehe ya Idi ul Fitri itaadhimishwa mwezi ujao.
    5. Wanafunzi watafanya mtihani wiki ijayo.
    Katika masimulizi ya matukio ya wakati ujao, maneno kama vile: kisha,

    halafu, mwishowe na baadaye hutumika.

    SOMO LA 8: Maadhimisho mbalimbali nchini Rwanda

    8.1 Shairi kuhusu maadhimisho mbalimbali nchini Rwanda

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha mtazame picha hizi

    na hapo baadaye msome na kukariri shairi lifuatalo na kulijadili:



    Maswali ya tathmini

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini na mjibu maswali haya ya
    tathmini kuhusiana na shairi mlilosoma hapo awali.

    1. Taja sherehe ambayo huadhimishwa mwanzoni mwa kila mwaka.
    2. Sikukuuu ya Mashujaa husherehekewa lini?
    3. Pasaka huadhimishwa na watu gani? Wao hukumbuka nini katika siku hii?
    4. Taja sikukuu za Waislamu kutokana na shairi ulilosoma?
    5. Sikukuu ya Uhuru nchini Rwanda husherehekewa lini?
    6. Kumbukumbu za mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi hufanyika lini?
    7. Shairi hili lina mishororo mingapi?
    8. Taja kibwagizo cha shairi hili.
    9. Sherehe za Krismasi huadhimishwa lini?

    10. Sikukuu ya Umuganura hufanyika lini?

    8.2 Msamiati kuhusu maadhimisho mbalimbali

    Kutokana na shairi mlilosoma hapo awali, katika makundi ya wanafunzi
    watatu watatu, jadilini maana ya msamiati mpya uliojitokeza unaohusiana na
    maadhimisho mbalimbali nchini Rwanda. Kamusi ya Kiswahili inaweza kutumika

    inapohitajika.

    Kwa mfano:

    Ukombozi: matendo au vita vya kuokoa watu kutoka kwenye hali mbaya

     yenye mateso au hali ya unyonge.

    Zoezi la 8.1

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mtunge sentensi
    sahihi kwa kutumia msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi zinazofuata.
    1. Leo tunaadhimisha sikukuu ya Mashujaa.
    2. Hii ni kalenda ya mwaka wa 2017.
    3. Mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwaka ni Januari.
    4. Wakristo husherehekea sikukuu ya Pasaka kila mwaka.
    5. Waislamu husali mara tano kwa siku.
    6. Waislamu huadhimisha sherehe ya Idi-ul-Fitr kila mwaka.
    7. Msimu wa sherehe za Krismasi umefika.
    8. Wanyarwanda huadhimisha sikukuu ya Uhuru wa Taifa kila mwaka.
    9. Leo ni tarehe kumi mwezi Disemba mwaka 2016.

    10. Sherehe ya Umuganura itaadhimishwa kesho

    8.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mjadiliane na
    kuelezana kuhusu:
    1. Shughuli zinazofanyika nyumbani kwenu wakati wa sherehe za mwaka
    mpya.
    2.  Namna mnavyoadhimisha sikukuu iliyo katika mwezi Julai.
    3. Shughuli zinazotekelezwa kwenu wakati wa sherehe za Umuganura.
    4. Shughuli zinazotekelezwa wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Ukombozi
    wa Taifa.
    5. Shughuli zinazofanyika wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Uhuru wa

    Taifa.

    8.4 Kusikiliza na kuzungumza: Zoezi la mazungumzo

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni mazungumzo mafupi

    yafuatayo na majibu yatolewe palipo na maswali mbele ya wanafunzi wenzenu.

    Mazungumzo kati ya Kamana na Teta:

    Kamana: Sikukuu ya Uhuru huadhimishwa tarehe gani?
    Teta: Sikukuu ya Uhuru huadhimishwa tarehe moja mwezi wa Julai kila
    mwaka.
    Kamana: Sikukuu ya sherehe za mwaka mpya huadhimishwa tarehe gani?
    Teta: Sherehe za mwaka mpya huadhimishwa tarehe moja mwezi wa
    Januari kila mwaka.

    Endelezeni mazungumzo haya kwa maneno yenu wenyewe. 

    8.5 Sarufi: Vitenzi vya silabi moja

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha mbainishe vitenzi

    vilivyo katika sentensi hizi zenye michoro.




    Zoezi la 8.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi tano sahihi kwa
    kutumia vitenzi vifuatavyo.
    Kwa mfano: kuja
    Jibu: Mwalimu alikuja kututembelea nyumbani kwetu.
    1. kufa
    2. kunywa
    3. kula
    4. kuwa

    5. kuja

    Maelezo muhimu!

    Katika lugha ya Kiswahili kuna vitenzi vyenye silabi moja. Vitenzi hivi
    huambatanishwa na ‘ku-’ katika matumizi.

    Kwa mfano:

    kufa:              –f 
    kuwa:            -w
    kunywa:      -nyw
    kula:              -l
    kuja:              -j

    Matumizi katika sentensi

    1. Mtoto alikunywa dawa.
    2. Ng’ombe alikula nyasi.

    3. Nyanya alikuja dukani.

    Zoezi la 8.3

    A. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, rekebisheni sentensi hizi:
    1. Mwalimu alija darasani.
    2. Mbuzi wetu alifa jana.
    3. Kalisa alinywa maji.
    4. Dada alila wali.
    5. Mama aliwa mgonjwa.

    B. Kanusha sentensi mlizosahihisha katika A hapo juu.

    8.5.1 Vitenzi vya silabi moja, tungo yakinishi na kanushi

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi hizi kisha
    mjadili ugunduzi wenu.

    1. Mtoto alikunywa dawa.                           - Mtoto hakunywa dawa.
    2. Paka wao alikufa jana.                             - Paka wao hakufa jana.

    3. Mgeni alikuja haraka.                               - Mgeni hakuja haraka.

    Maelezo muhimu!

    Vitenzi vya silabi moja huambatanishwa na ‘ku-’ katika hali yakinishi.
    Katika hali kanushi, vitenzi hivi huambatanishwa na kikanushi ‘ha-’ na

    nafsi husika. 

    Kwa mfano:
    1. Wagonjwa walikula chakula. - Wagonjwa hawakula chakula.
    2. Walimu walikunywa chai. - Walimu hawakunywa chai.

    3. Paka wa jirani walikufa jana. - Paka wa jirani hawakufa jana.

    Zoezi la makundi

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni mifano ya sentensi

    katika jedwali hili.


    Zoezi la 8.4

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tumieni vitenzi vyenye silabi
    moja vifuatavyo katika wakati uliopita hali yakinishi katika umoja na wingi.

    Tumieni nafsi zote za Kiswahili.

    Mfano: kunywa: -nyw

    Jibu: Mtoto alikunywa maziwa. - Watoto wali kunywa  maziwa.

    1. kuwa

    2. kuja
    3. kufa

    4. kula

    Zoezi la 8.5

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tumieni vitenzi vyenye silabi
    moja vifuatavyo katika wakati uliopita hali kanushi. Tumieni nafsi zote za
    Kiswahili.

    Mfano: kunywa: -nyw
    Jibu: Mtoto hakunywa maziwa yote.

    1. kuwa
    2. kuja
    3. kufa

    4. kula

    Zoezi la 8.6

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi zifuatazo
    katika umoja au wingi.
    Kwa mfano:
    Umoja: Mwalimu alikuwa darasani.
    Wingi: Walimu walikuwa madarasani.
    1. Mtu huyu alikuja jana jioni.
    2. Wanafunzi hawa wanakunywa maziwa.
    3. Mtoto anakula mkate.
    4. Panya alikufa mtegoni.

    5. Viongozi walikuwa mjini Kigali.

    SOMO LA 9: Matumizi ya kalenda ya mwaka

    9.1 Mazungumzo kuhusu matumizi ya kalenda ya mwaka

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tazameni kalenda hii ya mwaka wa
    2017 kisha msome mazungumzo yaliyo hapo chini na hatimaye mjibu maswali

    yanayofuata.

      


    Maswali ya ufahamu

    1. Mwezi wa Januari una Jumapili ngapi?
    2. Tarehe 5 mwezi wa Mei ni siku gani?
    3. Mwaka wa 2017 una siku ngapi?
    4. Mwezi wa Septemba una Jumatano ngapi?
    5. Sikukuu ya Mashujaa wa Taifa iliadhimishwa siku gani katika kalenda
    iliyo hapo juu?
    6. Krismasi itaadhimishwa siku gani katika kalenda iliyo hapo juu?
    7. Sikukuu ya mwaka mpya 2017 iliadhimishwa siku na tarehe gani?
    8. Mwezi wa Agosti una siku ngapi?
    9. Mwezi wa Disemba una Alhamisi ngapi?
    10. Ni miezi mingapi isiyokuwa na sikukuu katika kalenda iliyo hapo juu?

    Itaje.

    9.2 Msamiati kuhusu kalenda ya mwaka

    Zoezi la 9.1

    (i) Kutokana na mazungumzo kuhusu matumizi ya kalenda ya mwaka
    mliyoyasoma hapo awali, katika makundi ya wanafunzi watatu watatu,
    jadilini kuhusu maana ya msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi
    zinazofuata. Kamusi ya Kiswahili inaweza kutumika inapohitajika.

    1. Jumamosi ni siku inayotangulia Jumapili.
    2. Huu ni mwezi wa Ramadhani.
    3. Siku hii imekuwa ya mikutano mingi.
    4. Mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwaka ni Januari.
    5. Mwaka ujao tutazuru nchi ya Kenya.
    6. Sherehe za Krismasi hufanyika mwezi wa Disemba.
    7. Tarehe mbili mwezi ujao tutasafiri kuelekea kijijini kwetu.
    8. Tutafungua shule mwezi Mei.
    (ii) Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa

    kutumia msamiati uliopigiwa mistari katika Zoezi la 1 (i) hapo juu.

    9.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha mtazame mchoro

    ufuatao wa kalenda ya mwaka wa 2017 na kuijadili. 


    Katika makundi yenu, jadilini kuhusu namna ya kuisoma kalenda hiyo ya mwaka
    wa 2017 na kuielewa kimatumizi. Waelezee wenzako:
    1. Miezi yote iliyo na siku thelathini.
    2. Miezi yote iliyo na siku thelathini na moja.
    3. Mwezi ulio na siku chache kuliko miezi mingine.
    4. Miezi iliyo na Jumapili nyingi kuliko mingine.
    5. Miezi iliyo na sikukuu au matukio rasmi ya kitaifa ya kusherehekewa.
    6. Mwezi wa Disemba una Jumapili ngapi?
    7. Tarehe ya kwanza katika mwezi wa Septemba ni siku gani?

    8. Tarehe kumi mwezi wa Agosti ni siku gani?

    Maelezo muhimu!

    Kalenda ni kifaa kinachoonyesha siku, tarehe na miezi katika mwaka.
    • Mwaka una miezi kumi na miwili ambayo ni: Januari, Februari,
    Machi, Aprili, Mei, Juni, Julai, Agosti, Septemba, Oktoba,
    Novemba na Disemba.
    • Siku katika kila mwezi huanzia Jumapili hadi Jumamosi.
    • Mwaka mmoja una wiki hamsini na mbili.
    • Wiki moja ina siku saba ambazo ni: Jumapili, Jumatatu, Jumanne,
    Jumatano, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi.
    • Katika kalenda, siku za Jumapili huandikwa kwa kutumia wino wa
    rangi tofauti.
    • Siku za matukio makuu ya sherehe za kitaifa na kijamii huandikwa

    kwa kutumia wino wa rangi tofauti.

    9.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha mwigize mazungumzo
    mliyoyasoma hapo awali kati ya Birasa na Kalisa kuhusu matumizi ya kalenda ya

    mwaka.

    9.5 Sarufi

    Matumizi ya herufi kubwa na alama za uandishi

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni kifungu kifuatacho kisha
    mbainishe maneno yote yaliyotumia herufi kubwa pamoja na alama mbalimbali

    za uandishi na hapo baadaye mjibu maswali ya tathmini yanayofuata. 


    Maswali ya tathmini
    1. Eleza matumizi mbalimbali ya herufi kubwa kutokana na kifungu kifupi
    mlichosoma hapo awali kumhusu Biruta.
    Kwa mfano: Biruta anaishi Gikondo.
    Matumizi: Herufi kubwa imetumika mwanzoni mwa jina la mtu
     (Biruta) na jina la mahali (Gikondo).
    2. Eleza matumizi mbalimbali ya alama nyingine za uandishi kutokana na
    kifungu mlichosoma hapo juu kisha mwonyeshe matumizi katika sentensi.
    Kwa mfano: Nukta (.)
    Matumizi: Nukta imetumika mwishoni mwa sentensi kamili.
    Mfano wa sentensi: Biruta ni mwalimu mkuu katika shule ya

     sekondari ya Kamashashi iliyo mjini Kigali.

    Zoezi la 9.2

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, rekebisheni sentensi zifuatazo
    kwa kutumia alama za uandishi kwa usahihi.
    Kwa mfano: neza ataenda shule jumatatu
    Jibu: Neza ataenda shule Jumatatu.
    1. kwa nini ulichelewa shuleni
    2. lo umebeba mzigo huo pekee yako
    3. mama alienda sokoni kununua ndizi machungwa viazi na nanasi
    4. paka amekunywa maziwa

    5. ngabo atakuja lini

    Zoezi la 9.3

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, rekebisheni kifungu hiki kwa
    kutumia alama za uandishi pamoja na herufi kubwa kwa usahihi.

    siku moja nilienda sokoni kununua ndizi sukari samaki mboga na
    machungwa. njiani nilikutana na rafiki yangu birasa. alishangaa kuniona
    na kusema ah kumbe wewe pia huja sokoni nikamjibu kuwa mimi hupenda
    kumsaidia mama kununua bidhaa mbalimbali. nilimuuliza umekuja

    kununua nini. akanijibu kuwa alikuja kununua mboga na samaki

    Tathmini ya mada ya 2

    Zoezi la 1

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mjadili maswali
    yafuatayo. Waelezee wenzako kuhusu:
    1. Shughuli zinazofanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka kwa Wakristo.
    2. Shughuli zinazofanyika wakati wa sikukuu ya Idi ul Fitri kwa Waislamu.
    3. Shughuli na burudani zinazofanyika katika sherehe ya harusi.
    4. Sherehe ya Kiislamu ya Idi ul Adha huadhimishwa lini? Jadili shughuli
    zinazofanyika wakati wa sherehe hiyo.
    5. Sherehe ya Kikristo ya Krismasi huadhimishwa lini? Jadili shughuli

    zinazofanyika wakati wa sherehe hiyo.

    Zoezi la 2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, rekebisheni sentensi zifuatazo
    kwa kutumia alama za uandishi kwa usahihi
    kwa kutumia alama za uandishi kwa usahihi
    Kwa mfano: pasaka iliadhimishwa tarehe gani
    Jibu: Pasaka iliadhimishwa tarehe gani?
    1. baadhi ya sherehe katika kalenda yetu ni pasaka krismasi na umuganura
    2. siku ya kwanza ya wiki ni jumapili katika kalenda ya mwaka
    3. kamana anaishi wapi
    4. lo simu yangu imeanguka majini

    5. kilo moja ya chumvi huuzwa faranga mia mbili 200

    Zoezi la 3

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi zifuatazo
    katika wakati ujao.
    Kwa mfano: Baba alinunua maji, soda na mkate.
    Jibu: Baba atanunua maji, soda na mkate.
    1. Mwalimu alitufundisha Hisabati.
    2. Ng’ombe alikunywa maji mengi.
    3. Babu alitusimulia hadithi nzuri.
    4. Sikukuu ya Krismasi iliadhimishwa kwa sherehe kubwa.

    5. Manzi alinunua vitabu na kalamu.

    Zoezi la 4

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi kwa kutumia
    vitenzi vya silabi moja vifuatavyo katika wakati uliopita hali kanushi.
    Kwa mfano: kuja
    Jibu: Mwalimu hakuja shuleni jana.
    1. kunywa
    2. kula
    3. kuwa
    4. kuja

    5. kufa

    Zoezi la 5

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tajeni majina ya alama za

    uandishi zifuatazo kisha mtunge sentensi moja kwa kila alama. 

    Kwa mfano: .
    Jibu: Nukta
    Sentensi: Tutaadhimisha sikukuu ya Ukombozi mwezi Julai.
    1. ?
    2. !
    3. ,
    4. :
    5. egg

    6.

    Zoezi la 6

    Katika makundi ya wanafunzi watano watano, wasimulie wenzako kuhusu

    sikukuu yoyote mliyoadhimisha kwa kuzingatia wakati uliopita.

    Zoezi la 7

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa
    kutumia vitenzi vifuatavyo katika hali yakinishi na hali kanushi kwa kuzingatia

    wakati ujao. 

    Kwa mfano:                                                     andika
    Jibu:                                                                    (Yakinishi): Mwanafunzi ataandika ubaoni.
                                                                                    (Kanushi): Mwanafunzi hataandika ubaoni.
    1. sherehekea
    2. kula
    3. adhimisha
    4. kunywa

    5. soma

    Zoezi la 8

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, rekebisheni kifungu hiki kwa
    kutumia alama za uandishi pamoja na herufi kubwa kwa usahihi.

    sikukuu ya mwaka mpya huadhimishwa tarehe moja januari siku ya
    mashujaa huadhimishwa tarehe moja mwezi februari je wewe uliadhimisha
    sikukuu ya mwaka mpya kwa njia gani waislamu wana sherehe mbili kuu
    ambazo ni idi ul fitri pamoja na idi ul adha Wakristo vilevile wana sherehe
    mbili kuu ambazo ni krismasi pamoja na pasaka je wewe husherehekea

    sikukuu gani ya kidini.

    Zoezi la 9

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu,
     rekebisheni sentensi hizi kwa kutumia alama

     za uandishi pamoja na herufi kubwa kwa usahihi.

    1. rais aliongoza sherehe ya siku ya uhuru katika uwanja wa gikondo
    2. je wewe ulihudhuria sherehe ya umuganura mwaka jana

    3. lo sikujua unaweza kuimba vizuri hivyo kwenye sherehe hiyo

    SURA YA KWANZA : MADA KUU 1: LUGHA NA MAZINGIRASURA YA TATU: MADA KUU 3: UKUZAJI WA MATUMIZI YA LUGHA KIMAZUNGUMZO