SURA NINE: MADA KUU 4: UIMARISHAJI WA STADI YA UANDISHI NA MASIMULIZI KUPITIA LUGHA YA KISWAHILI
MADA KUU 4: UIMARISHAJI WA STADI YA
UANDISHI NA MASIMULIZI
KUPITIA LUGHA YA KISWAHILI
Mada Ndogo: Utungaji wa insha
SOMO LA 13: Sehemu kuu za insha
13.1 Kifungu kuhusu somo la Kiswahili
Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni michoro hii kisha msome
kifungu cha habari kilicho hapo chini na kujibu maswali ya ufahamu yanayofuata.


Maswali ya ufahamu
Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, someni tena kifungu kilicho hapo
juu kisha mjibu maswali yafuatayo.
1. Wanafunzi wa shule ya Mtume Paulo walimpenda mwalimu yupi?
2. Taja tabia za Bwana Gasimba.
3. Mtu ambaye ni mcheshi ni mtu mwenye tabia ya aina gani?
4. Kwa nini somo la insha liliwafurahisha wanafunzi?
5. Katika insha, mada na utangulizi huhusu nini?
6. Katika insha mwili wa insha huhusu nini?
7. Mwanafunzi anahitajika kuandika nini katika hitimisho la insha?
8. Je, umejifunza nini kutokana na kifungu hiki?13.2 Msamiati kuhusu sehemu za insha
Kutokana na kifungu cha habari ulichosoma hapo juu, katika makundi ya
wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu maana ya msamiati mpya uliojitokeza
unaohusiana na sehemu za insha. Kamusi ya Kiswahili inaweza kutumika
panapohitajika.
Kwa mfano:
mada – neno au sentensi ambayo inatambulisha jambo linalozungumziwa
katika insha iliyoandikwa. Aghalabu mada ya insha huwa haizidi manenomanane.
Zoezi la 13.1
A. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni maana ya
msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi zinazofuata kulingana na jinsi
ulivyotumika katika kifungu cha habari mlichosoma hapo awali.
1. Somo la Kiswahili litaanza kesho saa mbili asubuhi.
2. Mutoni aliandika insha bora kuliko wanafunzi wenzake.
3. Utangulizi wa insha yako unavutia.
4. Mwili wa insha hubeba ujumbe wa insha nzima.
5. Sharti kila insha iwe na hitimisho.
6. Masimulizi ya mwalimu wetu yalitufurahisha darasani.
B. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwakutumia maneno yaliyopigiwa mistari katika Zoezi 1A lililo hapo juu.
Maelezo muhimu!
Sehemu kuu za insha ni:
1. Mada au kichwa cha insha
Mada ya insha hutambulisha jambo linalozungumziwa katika insha.
Mada ya insha haifai kuzidi maneno manane. Mara nyingi mada ya
insha huandikwa kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari. Lazima mada
iwe na mvuto kwa msomaji.
2. Utangulizi au mwanzo wa insha
Utangulizi wa insha mara nyingi huwa ni aya moja tu. Unafaa kuvutia
kwa kiwango cha juu ili kumpa msomaji hamu ya kutaka kusoma insha
nzima.
3. Mwili wa insha
Hii ndiyo sehemu muhimu sana kwa sababu inabeba ujumbe kamili wa
insha nzima. Aya nyingi huandikwa hapa na ni bora aya hizi ziandikwe
kwa namna ya kutiririsha matukio kuanzia mwanzo hadi mwisho wa
insha.4. Hitimisho au mwisho wa insha
Sehemu hii huwa na sentensi chache tu katika aya moja. Hitimisho
hufupisha yaliyoandikwa katika mwili wa insha kwa namna ya kuvutiamsomaji.
13.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano
Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha mjadili kuhusu
sehemu kuu za insha mnazozifahamu. Hakikisheni kuwa mmejibu maswali haya.
1. Mada ya insha huhusu nini?
2. Utangulizi wa insha huandikwa kwa kuzingatia mambo gani?
3. Mwili wa insha huhusu nini?
4. Hitimisho huandikwa vipi?5. Lugha inayotumika kuandika insha huwa ya aina gani?
13.4 Kusikiliza na kuzungumza: Somo la imla
Zoezi la Imla
Sikiliza kwa makini sentensi utakazosomewa na mwalimu wako kisha
uzinakili katika daftari lako kwa kuzingatia alama sahihi za uandishi.
13.5 Sarufi
Ngeli ya U-ZI
Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha msome aya ifuatayona mworodheshe majina yaliyo katika ngeli ya U-ZI.
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi katika umoja na
wingi kwa kutumia maneno mliyoorodhesha hapo juu.
Maelezo muhimu!
Majina katika ngeli ya U-ZI katika sentensi hutumia kiambishi nafsi ‘u-‘
katika umoja na kiambishi nafsi ‘zi-‘ katika wingi.
Kwa mfano:
1. Ukuta wa nyumba yangu umepakwa rangi.
Kuta za nyumba zetu zimepakwa rangi.
2. Wimbo mzuri umeimbwa na mtoto.
Nyimbo nzuri zimeimbwa na watoto.Mifano ya majina na michoro yake katika ngeli ya U-ZI
A. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kanusheni sentensi zifuatazo.

Kwa mfano: Ufunguo mpya umepotea.
Jibu: Ufunguo mpya haujapotea.
1. Ulimi wake umepona.
2. Upanga huu utatumika kukatia muwa.
3. Uzi wangu umekatika.
4. Ukucha wako umeumia.
5. Wimbo mrefu utaimbwa na wanafunzi.
B. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi mlizokanushahapo juu katika wingi.
Zoezi la 13.2
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi katika
umoja na wingi kwa kutumia majina yafuatayo katika hali yakinishi.
Kwa mfano: Fito
Jibu: Ufito mrefu utatumiwa kujengea nyumba.
Fito ndefu zitatumiwa kujengea nyumba.
1. kurasa
2. ndevu
3. wakati
4. nyembe
5. upanga6. ulimi
Zoezi la 13.3
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, kanusheni sentensi mlizotunga
katika zoezi la 13.2 lililo hapo juu.
13.5.1 Ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi vya sifa
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini sentensi zinazofuata (zenyemichoro na picha) kisha mwelezane maneno yaliyopigiwa mistari ni ya aina gani.
Maelezo muhimu!

Maneno ambayo hutumiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu nomino huitwa
vivumishi. Vivumishi vinavyoeleza namna nomino inavyoonekana na
tabia ya nomino huitwa vivumishi vya sifa.
Mifano:
1. Ukuta mrefu umejengwa.
2. Uso safi umepakwa mafuta.
3. Ukucha mchafu utakatwa.4. Ufagio mpya utanunuliwa.
Zoezi la 13.4
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tambueni vivumishi vya sifa
katika sentensi zinazofuata.
Kwa mfano: Ufito mrefu umekatwa.
Jibu: ‘mrefu’ ni kivumishi cha sifa
a) Wimbo mzuri umeimbwa na wanafunzi hawa.
b) Ukurasa mweupe umechafuliwa na mtoto yule.
ch) Fagio mpya zitauzwa sokoni na mama yangu.
d) Uzi mweusi utatumiwa kushonea nguo yake.e) Ndevu ndefu zitanyolewa kesho.
Zoezi la 13.5
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi sahihi kwa
kutumia majina ya ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi hivi.
Kwa mfano: -refu
Jibu: Waraka mrefu umeandikwa na Kabera.
1. -chafu
2. safi
3. -eusi
4. -kubwa5. -dogo
SOMO LA 14: Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa insha
14.1 Kifungu kuhusu malezi bora
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro ifuatayo kisha
mjadili na mwelezane mnachokiona na hapo baadaye msome kifungu cha habarikilicho hapo chini na kujibu maswali yanayofuata.

Maswali ya ufahamu
1. Eleza tabia za wazazi wa Mutesi.
2. Mutesi ameiga tabia zipi kutoka kwa wazazi wake?
3. Taja mambo muhimu ya kuzingatia katika kuandika insha.
4. Malezi bora ni nini?
5. Umejifunza nini kutokana na kifungu ulichosoma hapo juu?
Maswali ya uhakiki
1. Kifungu ulichosoma kina aya ngapi?
2. Taja majina ya watu waliozungumziwa katika kifungu ulichosoma.
3. Eleza tabia za watu uliowataja kutokana na kifungu ulichosoma.
4. Eleza mawazo makuu yanayozungumziwa katika kila aya.5. Onyesha aya zinazojenga kila sehemu kuu ya insha uliyosoma.
Maelezo muhimu!
• Mkusanyiko wa sentensi ambazo zinazungumzia wazo moja kuu
huitwa aya.
• Ili aya ieleweke, sharti mwandishi atumie kwa usahihi alama za
uandishi kama vile: nukta, koma, mkato, herufi kubwa, n.k.
14.2 Msamiati kuhusu uandishi wa insha
Kutokana na kifungu cha mazungumzo ulichosoma hapo awali, katika makundi
ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu maana ya msamiati mpya
uliojitokeza na kuhusiana, kisha utunge insha. Kamusi ya Kiswahili inaweza
kutumika inapohitajika.
Kwa mfano:
insha – mtungo unaoandikwa kuhusu kitu, mtu au jambo kwa kufululiza
maneno katika sentensi hadi katika aya kwa njia ya kusimulia au
kuhadithia jambo fulani hatua kwa hatua.
Zoezi la 14.1
A. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni maana ya
msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi zinazofuata kulingana na jinsi
ulivyotumika katika kifungu mlichosoma hapo awali.
1. Mwalimu ameandika aya mbili za insha kwenye ubao.
2. Mada ya insha aliyotupa mwalimu wetu ni rahisi.
3. Sharti ubuni kisa akilini kabla ya kuandika insha.
4. Insha nzuri inafaa kutiririka kutoka mwanzo hadi mwisho.
5. Kila mwanafunzi anashauriwa kuwa na mwandiko safi.
6. Mwalimu wetu hukosoa makosa yote ya kisarufi.
7. Ni jukumu la kila mzazi kumpa mwanawe malezi mema.
8. Mutesi aliziiga tabia nzuri za wazazi wake.
B. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi kwa kutumia
msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi za zoezi la 1A lililo hapo juu.
Maelezo muhimu!
Insha ni mtungo unaoandikwa kuhusu kitu, mtu au jambo kwa
kufululiza maneno katika sentensi hadi katika aya kwa njia ya kusimulia
au kuhadithia jambo fulani hatua kwa hatua. Insha inaweza kuandikwakatika mpango wa mazungumzo.
Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa insha
1. Mwandiko uwe safi: Maandishi yaonekane vizuri na yasomeke ili
kurahisisha usomaji.
2. Urefu: Insha iwe na urefu wa wastani (insha isiwe fupi sana na
isiwe ndefu sana).
3. Lugha ya insha: Sharti lugha sahihi, sanifu na rahisi kuelewekaitumike ili kumvutia msomaji.
4.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano
Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha mjadili kuhusu
mambo ambayo nyinyi huzingatia katika kuandika insha mbalimbali. Wanafunzi
waelezane:
1. Mada mbalimbali za insha mbalimbali.
2. Mambo wanayozingatia wanapoandika insha.
3. Namna ya kuboresha mwandiko usiofaa.
4. Kiasi cha urefu wa kuandika insha mbalimbali.5. Mapambo mbalimbali yanayoweza kutumika katika kuandika insha.
14.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu namna ya kuandikainsha bora kwa kuzingatia kifungu mlichosoma hapo awali.
14.5 Sarufi
Ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi viashiria
Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni michoro ifuatayo kishamuilinganishe na sentensi zilizo chini yake.


Zoezi la 14.2
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni wingi wa sentensi
zinazofuata.
1. Ukuta huu umekamilika kujengwa.
2. Uso huo una kidonda.
3. Ufagio ule umetumika kwa muda mrefu.
4. Uzi huu unahitajika na mama.
5. Wimbo huo unavutia.
6. Wembe ule ulimkata mtoto.Je, mmegundua nini?
Maelezo muhimu!
Maneno ambayo hutumiwa kuonyesha umbali wa nomino huitwa
vivumishi viashiria. Yaani ni maneno yanayoashiria iliko nomino.
Kuna umbali wa aina tatu:
a) Karibu na mzungumzaji
Kwa mfano: Ukuta huu, uso huu, uzi huu n.k.
b) Mbali kidogo na mzungumzaji
Kwa mfano: Ukuta huo. uso huo. uzi huo n.k.
ch) Mbali sana na mzungumzajiKwa mfano: Ukuta ule, uso ule, uzi ule n.k
Vivumishi viashiria katika wingi hutegemea umbali wa nomino
inayorejelewa:
a) Katika ngeli ya U-ZI, nomino ikiwa karibu na mzungumzaji, katika
umoja kivumishi kiashiria kitakuwa ‘huu’ na katika wingi kitakuwa
‘hizi’.
b) Katika ngeli ya U-ZI, nomino ikiwa mbali kidogo na mzungumzaji,
katika umoja kivumishi kiashiria kitakuwa ‘huo’ na katika wingi
kitakuwa ‘hizo’.
ch) Katika ngeli ya U-ZI, nomino ikiwa mbali sana na mzungumzaji,
katika umoja kivumishi kiashiria kitakuwa ‘ule’ na katika wingikitakuwa ‘zile’.
Zoezi la 14.3
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni umoja wa sentensi hizi.
1. Kurasa hizi zimelowa maji.
2. Kucha hizi zitakatwa.
3. Funguo hizo ni za nyumba za walimu wetu.
4. Panga hizi zitatumika shambani.5. Nyimbo hizo zinaimbwa vizuri sana.
Zoezi la 14.4
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizo wazi kwa
kuchagua vivumishi viashiria sahihi kutoka kwenye mabano.
1. Ukuta __________ umebomolewa. (zile, ule)
2. Fito __________ zimevunjika. (hizo, hiyo)
3. Nyuzi ___________ za manjano zimeuzwa. (ile, zile)
4. Uso ___________ umevimba. (huu, hii)5. Nyembe __________ zitawakata watoto wale. (ile, zile)
Zoezi la 14.5
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi sahihi kisarufi
kwa kutumia majina yafuatayo ya ngeli ya U-ZI.
1. Wimbo
2. Waraka
3. Ukuta
4. Udevu5. Unywele
SOMO LA 15: Aina mbalimbali za insha
15.1 Kifungu kuhusu umuhimu wa adabu
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro hii kisha
mwelezane mnachokiona. Tangulizeni sentensi zenu kwa: Mimi ninaona…Hapo
baadaye msome kifungu cha habari kilicho hapo chini na kujibu maswali yaufahamu yanayofuata.

Maswali ya ufahamu
1. Eleza sifa za Mutoni.
2. Eleza hali ya familia ya Mutoni.
3. Kwa nini mwalimu wa somo la Kiswahili aliamua kumfadhili Mutoni?
4. Kwa nini wanafunzi walimpenda Mutoni?5. Kozi ambayo Mutoni aliifanya chuoni ilikuwa na manufaa gani?
Maswali ya uhakiki
1. Eleza namna mada inavyohusiana na insha uliyosoma.
2. Eleza mawazo makuu matatu yaliyojitokeza katika insha uliyosoma.
3. Andika mawazo hayo kwa maneno yako mwenyewe. Usizidi manenosabini (70).
15.2 Msamiati kuhusiana na umuhimu wa adabu
Kutokana na kifungu mlichosoma hapo awali, katika makundi ya wanafunzi
wanne wanne, jadilini kuhusu maana ya msamiati mpya. Kamusi ya Kiswahili
inaweza kutumika panapohitajika.
Kwa mfano:wema - mambo mazuri anayoyafanya mtu
Zoezi la 15.1
A. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, elezeni maana ya msamiati
uliopigiwa mistari katika sentensi zinazofuata kulingana na jinsi
ulivyotumika katika kifungu mlichosoma hapo awali.
1. Mutoni anasoma katika kidato cha tatu.
2. Baba yangu amelipa karo yote ya muhula huu.
3. Mimi sina mahitaji mengi nyumbani.
4. Wao wanaishi katika kijiji duni.
5. Mama yangu ni mpole na mwenye bidii.
6. Mutoni ndiye kiranja mkuu katika shule yao.
7. Sare za wanafunzi hawa ni mpya.
8. Ufadhili aliopata kaka yangu uliwafurahisha wazazi wetu.
9. Kamana anasomea kozi ya udaktari chuoni.
B. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi sahihi kwakutumia maneno yaliyopigiwa mistari katika sentensi za Zoezi la 1A.
15.3 Matumizi ya lugha: Mifano ya insha
15.3.1 Insha ya wasifu
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tazameni michoro hii kisha msomemfano wa insha ifuatayo na mjadili maswali yanayofuata:

Maswali ya uhakiki
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini maswali yanayofuata
kutokana na mfano wa insha ya wasifu uliotolewa hapo juu.
1. Eleza insha mliyosoma ni ya aina gani.
2. Eleza mambo ya kuzingatia katika kuandika insha ya aina hii.
3. Pendekeza kichwa cha insha hii.
4. Eleza sifa ambazo ni za kimaumbile za baba anayezungumziwa katika
insha mliyosoma.
5. Taja tabia za baba anayezungumziwa katika insha mliyosoma hapo juu.
6. Kwa nini watu wengi wanampenda baba huyu?7. Ni nini kinachoonyesha kuwa baba huyu ana bidii katika kazi yake?
Maelezo muhimu!
Insha zinazoeleza sifa nzuri au mbaya kuhusu maumbile ya mtu au kitufulani huitwa insha za wasifu.
Zoezi la kuandika
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni insha ya wasifu wakobinafsi.
15.3.2 Insha ya mazungumzo
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni mchoro huu kisha msomemfano wa insha ifuatayo na mjadili maswali yanayofuata:
Maswali ya uhakiki

Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini maswali haya kutokana
na mfano wa insha mliyoisoma hapo juu.
1. Eleza insha mliyosoma ni ya aina gani.
2. Eleza mambo ya kuzingatia katika kuandika insha ya aina hii.
3. Pendekeza kichwa cha insha hii.
4. Wazungumzaji katika mazungumzo haya ni kina nani?
5. Eleza kazi ya daktari katika jamii.
6. Daktari anamsaidia vipi Kayitesi?7. Kayitesi anaugua wapi?
Maelezo muhimu!
Insha zinazohusu mazungumzo kati ya watu wawili au zaidi huitwainsha za mazungumzo. Insha hizi huandikwa kwa mtindo wa tamthilia.
Zoezi la maigizo
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, igizeni mazungumzo kati ya Daktarina Mgonjwa (Kayitesi) mliyosoma hapo awali.
Zoezi la kuandika
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, bunini mazungumzo kati yamwalimu na mwanafunzi kisha myaigize.
15.4 Kusikiliza na kuzungumza
Somo la imla
Sikiliza kwa makini sentensi ambazo mwalimu wako atakusomea kisha uziandikekwa usahihi katika daftari lako.
15.5 Sarufi
Ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi vimilikishi
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni picha na michoroifuatayo kisha muiambatanishe na sentensi zilizo chini yake.


Mifano katika sentensi
Umoja Wingi
1. Wimbo wangu unavutia. Nyimbo zetu zinavutia.
2. Ukuta wangu umepakwa rangi. Kuta zetu zimepakwa rangi.
3. Unywele wako utanyolewa kesho. Nywele zenu zitanyolewa kesho.
4. Uso wako umevimba. Nyuso zenu zimevimba.
5. Uzi wake umepotea. Nyuzi zao zimepotea.6. Ukurasa wake umeandikwa. Kurasa zao zimeandikwa.
Zoezi la 15.2
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa kutumia
majina yafuatayo pamoja na vivumishi vimilikishi vilivyo kwenye mabano.
Kwa mfano: Wimbo (wake)
Jibu: Wimbo wake ulipendwa na wasikilizaji wote.
1. Kurasa (zetu)
2. Ufa (wako)
3. Nyuzi (zenu)
4. Ufito (wangu)5. Nyembe (zao)
Zoezi la 15.3
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi zifuatazo katika
wingi.
Kwa mfano: Waraka wangu umetumwa.
Jibu: Nyaraka zetu zimetumwa.
1. Ubao wake umepakwa rangi nyekundu.
2. Ukuta wako umeangukia nyumba yangu.
3. Ukucha wangu umeumia vibaya.
4. Wakati wako umekwisha.5. Wimbo wake ulirekodiwa jana mjini Kigali.
Zoezi la 15.4
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi zifuatazo katika
umoja.
Kwa mfano: Nyembe kali zitatumika kukata kucha.
Jibu: Wembe mkali utatumika kukata ukucha.
1. Ndevu za wavulana wale zimekuwa ndefu sana.
2. Nywele za mabinti hawa ni nyeusi tititi.
3. Nyayo za watoto hao zina matope.
4. Nyakati za kusoma kwa wanafunzi zimekwisha.5. Nyuso za wazee wale zimepakwa mafuta.
Zoezi la 15.5
Andika wingi wa majina haya ya ngeli ya U-ZI.
1. Wayo
2. Wakati
3. Wimbo
4. Ufito5. Upinde
SOMO LA 16: Aina za insha
16.1 Kifungu kuhusu madhara ya uvivu
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni mchoro ufuatao
kisha mjadili kuhusu kinachoendelea katika mchoro wenyewe. Hapo baadaye,
msome kifungu kilicho hapo chini kuhusu madhara ya uvivu na mjibu maswaliyanayofuata.



Maswali ya ufahamu
1. Eleza maana ya uvivu.
2. Eleza madhara ya uvivu.
3. Uvivu huathiri mwanafunzi kwa namna gani?
4. Nchi huathirika vipi kutokana na uvivu?
5. Afya za watu wavivu huweza kuathirika kwa njia gani?
6. Umejifunza nini kutokana na kifungu ulichokisoma?7. Eleza namna ya kuepukana na uvivu.
16.2 Msamiati kuhusu madhara ya uvivu
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya kutoka
katika kifungu mlichokisoma hapo juu na kuueleza. Zingatieni matumizi yamsamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale inapohitajika.
Zoezi la 16.1
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zifuatazo
kisha mtunge sentensi sahihi kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mstari.
1. Uvivu ni adui wa maendeleo kwa binadamu.
2. Dawa za kulevya huathiri afya ya mtu anayezitumia.
3. Umaskini na ujinga husababishwa na uvivu.
4. Mwanafunzi yule alifanya bidii katika masomo yake na akafaulu.
5. Usipojitahidi katika shughuli zako utaishia kuwa ombaomba.
6. Mtu mvivu huweza kujiingiza katika uhalifu.7. Kamana alijitahidi katika mtihani wake wa kitaifa.
Zoezi la 16.2
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kamilisheni sentensi zifuatazo
kwa kutumia maneno yafuatayo:
wasumbufu, dawa za kulevya, masomo, bidii, maendeleo,ombaomba.
Kwa mfano: Watu walio wavivu huishia kuwa _____________ sana
katika jamii.
Jibu: Watu walio wavivu huishia kuwa wasumbufu sana katika jamii.
1. ______________ wamejaa mjini.
2. Uvivu huathiri ______________ ya nchi.
3. Mwanafunzi mvivu hawezi kufanikiwa katika ______________ yake.
4. Ubakaji, ukorofi pamoja na matumizi ya ___________ yakomeshwe.
5. Mtu akifanya ___________ katika shughuli zake atafanikiwa.
16.3 Matumizi ya lugha: Aina za insha
16.3.1 Insha ya maelezo
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro hii kisha msomemfano wa insha ifuatayo na mjadili maswali yanayofuata:
Maswali ya uhakiki

1. Waeleze wenzako insha uliyosoma ni ya aina gani?
2. Mambo gani huzingatiwa katika kuandika insha ya aina hii?
3. Eleza umuhimu wa maji kwa binadamu.
4. Eleza umuhimu wa maji kwa mimea.
5. Wanyama hufaidika vipi kutokana na maji?6. Miti hutusaidia kwa njia ipi kupata maji?
Maelezo muhimu!
Insha ambazo hutoa taarifa kuhusu mtu, kitu, mahali, hali au jambo fulani
huitwa insha za maelezo. Insha hizi huhitaji maelezo ya kweli wala siyomaelezo ya kubuni.
Zoezi la kuandika
Andika insha ya maelezo kuhusu vivutio vya utalii katika nchi ya Rwanda.
16.3.2 Insha ya barua rasmi
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni mfano wa insha ifuatayokisha mjadili maswali yanayofuata.
Maswali ya uhakiki
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini maswali haya kwa
kurejelea mfano wa insha mliyosoma hapo juu.
1. Eleza insha mliyosoma ni ya aina gani.
2. Eleza mambo ya kuzingatia katika kuandika insha ya aina hii.
3. Pendekeza kichwa cha insha hii.
4. Anwani ngapi zimetumika katika barua hii? Ni za kina nani?5. Lengo la kuandika barua hii ni lipi?
Zoezi la kuandika/Utafiti
1. Tunga mfano wa barua ya kirafiki.
2. Eleza namna ya kuandika barua ya mwaliko. Buni mfano mmoja wa
barua ya mwaliko.
3. Ni mambo gani huzingatiwa katika kuandika:
i) Barua rasmi
ii) Barua ya kirafikiiii) Barua ya mwaliko
16.4 Kusikiliza na kuzungumza
Somo la imla
i) Sikiliza kwa makini insha ambayo mwalimu wako atakusomea kisha
uiandike katika daftari lako.
ii) Kwa kufuata mfano wa insha uliyosomewa na mwalimu wako, buni inshayako mwenyewe inayofanana na hiyo.
16.5 Sarufi
Ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi vya idadi
Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni michoro ifuatayo kishamuiambatanishe na sentensi zilizo chini yake

Je, mmegundua nini?
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu maneno yaliyopigiwa
mistari katika sentensi zilizo hapo juu. Maneno hayo ni ya aina gani? Maneno
hayo yanarejelea nini?Zoezi la 16.3
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa
kutumia majina yafuatayo pamoja na vivumishi vya idadi.
Kwa mfano: nyembe nane
Jibu: Mwalimu alinunua nyembe nane kutoka dukani.
1. Kuta (mbili) 2. Fagio (tatu) 3. Teo (nne)4. Uzi (mmoja) 5. Nyuso (tano) 6. Nyaraka (kumi)
Maelezo muhimu!
Maneno ambayo hutumiwa kutaja hesabu, idadi au kiasi cha vitu au
viumbe fulani huitwa vivumishi vya idadi.
Vivumishi vya idadi hugawika katika aina mbili:
i) Vivumishi vya idadi kamili, kwa mfano: ukuta mmoja,
kuta nne, uso mmoja, nyuso tano, upanga mmoja, panga
nane, n.k.
Mifano katika sentensi:
a) Uzi mmoja umepotea.
b) Nyuzi tano zimepotea.
ch) Ukuta mmoja umejengwa.
d) Kuta nne zimejengwa.
ii) Vivumishi vya idadi isiyo kamili, kwa mfano: kuta chache,kurasa nyingi, nyimbo kadhaa, nyaraka tele, n.k.
Mifano katika sentensi:
a) Nyimbo nyingi ziliimbwa jana.b) Nyaraka kadhaa zimepotea.
Zoezi la 16.4
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa
kutumia majina yafuatayo pamoja na vivumishi vya idadi.
1. Wimbo (mmoja)
2. Kurasa (nyingi)
3. Nyufa (mbili)
4. Uzi (mmoja)
5. Fito (kadhaa)6. Nyembe (chache)
Zoezi la 16.5
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jazeni nafasi zilizo wazi katika
sentensi zinazofuata kwa kutumia vivumishi vya idadi sahihi kutoka kwenye
mabano.
Kwa mfano: Nyaraka ____________ zimesomwa. (wanne, nne, zinne)
Jibu: Nyaraka nne zimesomwa.
1. Ulimi ____________ umeumia. (moja, mmoja, umoja)
2. Fito ____________ zitatumika kujengea. (nyingi, vingi, wingi)
3. Nyimbo __________ zimetungwa na baba yake. (chache, uchache,
wachache)
4. Nyuso ____________ zimepakwa mafuta. (tano, watano, vitano)5. Ufagio ____________ uliuzwa jana. (moja, mmoja, umoja)
Tathmini ya mada ya 4
Zoezi la 1
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi kwa
kutumia majina yafuatayo ya ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi vimilikishi
mlivyopewa kwenye mabano.
1. Wimbo (wao)
2. Kurasa (zake)
3. Nyufa (zetu)
4. Uzi (wangu)
5. Fito (zenu)
6. Nyembe (zako)
Zoezi la 2
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, kanusheni sentensi hizi.
1. Utepe wangu ulipotea.
2. Kucha zenu zinapendeza.
3. Upanga wake ulivunjika.
4. Wimbo wa taifa unaimbwa sasa.5. Wakati wa mapumziko umewadia.
Zoezi la 3
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi za zoezi la
2 lililo hapo juu katika umoja au wingi hali yakinishi.
Zoezi la 4
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tambueni vivumishi vya sifa
katika sentensi zifuatazo.1. Udevu mfupi hautakatwa.
2. Ukuta mpana utapakwa rangi.
3. Funguo nyepesi zimeanguka.
4. Wembe mzee ulinikata.
5. Ubao mweusi utatumika
Zoezi la 5
Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tungeni:
1. Wasifu kuhusu shule yako.
2. Mazungumzo kati ya mzazi na mtoto wake.
Zoezi la 6
Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, jadilini kuhusu madhara ya uvivu
katika jamii hasa kwa mwanafunzi.

